Select Menu

Makala

KILIMO BIASHARA

MKULIMA

UFUGAJI

UVUVI

PICHA ZA MAZAO

VIPINDI VYA RADIO

VIPINDI VYA RUNINGA-TV


Serikali ya Tanzania imesema pembejeo hafifu za kilimo wanazouziwa wakulima nchini zimechangia kudidimiza kilimo cha mazo ya chakula nchini na kusababisha kilimo kutokuwa na tija.




Serikali ya Tanzania imesema pembejeo hafifu za kilimo zinazouziwa wakulima nchini zimechangia kudidimiza kilimo cha mazo ya chakula nchini na kusababisha kilimo kutokuwa na tija.


Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Uvuvi, Dk. Florens Turuka Wakati akizindua mpango wa kuendeleza kilimo kwa wakulima wadogo wa mkoani Mbeya,
Akizindua Mpango huo unaowezeshwa na Serikali ya Norway Dk.Turuka amesema serikali itachukua hatua kwa Makampuni yanayouza pembejeo bandia zisizokidhi viwango katika sekta ya kilimo na kuchangia kudorora kwa uzalishaji wa mazao
Mpango huo umelenga kuwafikia wakulima 30,000 katika mkoa wa mbeya Ifikapo 2020 kupitia Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika AGRA,ambapo serikali ya Norway ilitoa Dola za kimarekani Bilioni 1.2 katika mpango wa awamu ya kwanza.


Kwa upande wake ,Naibu Waziri wa Mambo ya nje ya Norway Tony Skogen amesema serikali yake imelenga kumuinua mkulima mdogo ili kunufaika na kilimo na kuboresha maisha.


Nae Rais wa AGRA,Dkt.Agnes Kalibata anasema katika kila wanawake kumi saba wanategemea kilimo katika kumu maisha yao katika maeneo ya vijijini licha ya changamoto zinazowakabili.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Abbas Kandoro anasema wakulima nchini wa mazao ya chakula wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja kutofika kwa Pembejeo za kilimo kwa wakati,ukosefu wa mbolea.
- -
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku wa kuamikia leo katika Machinjio ya Ukonga Mazizi.

Katika ziara hiyo, Waziri Nchemba  amekamata ng’ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, na kati yao ni ng’ombe 20 tu ndo walikuwa na kibali cha kuchinjwa, hivyo ushuru  wa ng’ombe 180  ulikuwa  unatafunwa  na  watumishi  waovu.
"Nimekamata ng'ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, ni ng'ombe 20 tu kati ya hao 200 ndio wanakibali cha kuchinjwa,

Kwa maana hiyo ushuru wa ng'ombe 180 umekwenda mifukoni mwa watumishi waovu na wenye lengo baya dhidi ya serikali yetu.

Hivyo basi, nimewasimamisha kazi kuanzia mkuu wa mnada wa Pugu ambaye siku si nyingi aliaminiwa na serikali na kupewa jukumu ili aongoze mnada huo,watumishi wote waliotajwa kwenye ubadhilifu huo."
Alisema Mwigulu Nchemba 


Baada  ya  kubaini  hali  hiyo,Waziri Nchemba ameufukuza  uongozi wote  wa  machinjio  hayo  na  kuagiza  vyombo  vya  dola  viwakamate  viongozi  wote waliohusika  na  kuwafikisha  mahakamani.

- -


Miaka ya hivi karibuni kwenye Mikoa ya Arusha, Manyara, Iringa, Mbeya,Tanga, Singida na Kilimanjaro zao la vitunguu limejizolea umaarufu mkubwa kwa kuendelea kuajiri maelfu ya Watanzania. Kuna ambao wamefikia ndoto zao kupitia kilomo cha vitunguu, wamejenga nyumba, wamefungua makampuni yao, wanasomesha watoto nk. Vitunguu hivi hivi kuna rafiki zangu wamenunua magari ya ndoto zao, wamejipa likizo nchi za nje.

Nitaongelea hasa eneo la Ruaha Mbuyuni na Mahenge sehemu ninayolima mimi. Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa zao la vitunguu.Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia umwagiliaji.(Local Irrigation) Maji mengi hasa wakati wa masika husababisha magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa vizuri, hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao.

Aina ya mbegu tunayolima sisi pale Mahenge na Ruaha Mbuyuni ni pamoja na Mang’ola (traditional) red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia magunia 70- 90 kwa hekta ikiwa kilimo bora kitazingatiwa na iwapo mkulima atakuwa anaongozwa na malengo yake na hamasa ya ndani (self drive) Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia, soko, msimu wa kupanda nk. Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na maduka ya TFA, na maduka ya bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali. Ingawa wapo baadhi ya watu hasa maeneo ya Ilula –Iringa ambao huandaa wenyewe mbegu kwa kutumia maua ya vingunguu.

Uandaaji wa kitalu hutegemea sehemu husika, lakini kwa kifupi Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji na huchukua takribani wiki tano mpaka sita kabla ya kupelekwa kwenye shamba husika. Zipo changamoto mbalimbali ambazo hujitokeza kwenye maandalizi ya kitalu mpaka shambani, changamoto hizo ni pamoja na wadudu, ugonjwa wa ukungu, Wadudu waharibifu ni pamoja na Chawa wekundu ambao wanashambulia majani, na wadudu waitwao Sota ambao hukata miche. Ili kudhibiti tatizo, shamba likaguliwe mara kwa mara kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili za mashambulizi, mkulima – mjasirimali ana shauriwa kuchukua hatua za kuzuia kabla uharibifu mkubwa haujatokea ambao husabaisha wakulima wapya kukata tama na kurudi kule kule kwenye kuilamikia serikali kwamba haiwajali.

Baada ya maandalizi ya kitalu na mbengu kupelekwa shambani, hatua inayofatia ni ufatiliaji wa malakwamala kwa kupulizia dawa na palizi. Iwapo mkulima yupo mbali na eneo husika, kwa mfano yupo Mwanza, Dar, Moshi ama popote Duniani, mkulima atalazimika kuajiri vijana ambao watamfanyia kazi kwa malipo mpaka vitunguu vitakapo komaa. Miche ya vitunguu, huota taratibu sana, hivyo miezi ya mwanzoni, miche husongwa sana na magugu. Palizi mbili mpaka tatu zinashauriwa na zinatosha kuweka shamba safi.

Kabla ya kuanza kuvuna vitunguu mkulima anashauriwa kukagua shamba ili kuhakikisha kuwa vitunguu vimekomaa. Na iwapo upo mbali na shamba lako hakikisha unatembelea shamba lako malakwamala. Dalili ya vitunguu kukomaa ni, majani kunyauka na kuanza kukauka asilimia 80 -100% na majani kukauka. Mpaka sasa hapa Tanzania, vitunguu huvunwa kwa mikono. Mimea inangolewa au kuchimbuliwa kwa kutumia jembe dogo.

Baada ya kuvuna vitunguu vinaweza kuachwa shambani vikiwa vimefunikwa na majani kukinga jua kwa muda wa siku mbili au tatu kutegemeana na hali ya hewa. Lengo nikuimarisha ngozi(Nyama) ya vitunguu nk. Pia kupunguza unyevu kwenye majani na mashina na kuruhusu sehemu ya chini ya shingo kufunga. Ikiwa usalama ni mdogo, vitunguu vinachambuliwa na kukatwa majani na mizizi na kuanikwa sehemu nyingine. Ukaushaji hutumia wiki mbili kutegemea hali ya eneo.

Kwa sasa soko la vitunguu lipo juu sana,Watu wa kada mabalimabali wanahusika na ununuzi na uuzaji wa vitunguu wakiwa ni pamoja na: wakulima, wachuuzi, wafanya biashara ndogondogo, wauza jumla, wauza rejareja, wasafirishaji na madalali. Kutoka shambani mpaka sokoni.

Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, hekari moja inaweza kutoa magunia 80-100 kwa sasa maeneo ya Njombe, Iringa, na Kwingineko gunia moja la vitunguu huuzwa kati ya shilingi 130,000/= mpaka laki 150,000/= lakini mkoani Njombe kwa bei ya sasa gunia moja ni shilingi 200,000/= kwa gunia. Ingawa kuna baadhi ya misimu soko hushuka sana mpaka kufikia shilingi laki moja kwa gunia ama elfu 70.(Kumbuka kwamba kutafuta pesa ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu kadiri unavyo ucheza ndiyo unavyo kuwa hodari-uchaguzi ni wako) Ukiwa na gunia labda 70 ukaziuza unaweza pata hadi shilingi milioni milioni 9, kwa ekari moja baada ya kuondoa gharama yote. Sasa ukiwa na ekari 5, 6,ama 3 utakuwa na shilingi ngapi? Wakati huo unasubiri mshahara wako. Kaka yangu mimi kwa msimu uliopita alipata magunia 1000, ni utajiri gani huu?

Kila mtu anayo nafasi sawa (equal channce) ya kuwa na fedha za kutosha kumpa uhuru wa kiuchumi. Pili hakuna raha wala sifa ya kuendelea kuwa masikini, kama unafikiri nisifa ama unajidanganya kuwa masikini watapunguziwa adhabu siku ya mwisho unapoteza muda wako kwa sababu masikini ni mzigo kwa dunia. Masikini na umasikini wake hata awe ni mtakatifu na mwema kiasi gani ni kwamba anaitesa dunia (kwa sababu anahitaji kusaidiwa). Tajiri (ama niseme mwenye fedha za kutosha) hata kama ni mchoyo ama bahiri bado ni msaada kwa dunia (kwa sababu anajisaidia).

Ninatamani kila mmoja apokee changamoto ya kutamani kuwa na uhuru wa kifedha na kiuchumi kwa kuanza na vitu tunavyo viona ni vidogo kwenye macho yetu ama kuachana na kasumba tuliyopewa shuleni kwamba ukimaliza kusoma lazima usake ajira. Ajira zenyewe hakuna na zilizopo bado ni chache. Na hili linawezekana ikiwa mitazamo na imani za wengi kuhusu fedha zitabadilika na kuwa zinazosapoti badala ya kuvuruga nafasi ya mtu kupata fedha. Kila Mtanzania anastahili ushindi wa kifedha. Wengi wetu tumekuwa watu wa kuhangaikia malengo ya wenzetu, kuna watanzania wenzetu wapo tayari kuzungumzia Malengo za timu za ulaya siku nzima, wiki, mwezi na jinsi ya kuhakikisha wanapata ushindi n.k., mtu huyohuyo hana ajira, ama aliyonayo mshahara hautoshi.

Kwa watanzania watakao penda kufanya kilimo hiki ama kile cha miti wanaweza kunitafuta nikawapa maelezo ya kutosha. Nchi hii ina matatizo mawili ya msingi kwenye kipengele cha Ujasiriamali, kuna wanaozifahamu fursa lakini hataki kuziweka wazi, sijuwi wanaogopa nini? Labda wana hofu ama ni wachoyo. Pia, kuna wale ambao walishazisikia fursa lakini bado wanasema nitaanza kesho na wapo wale wanaosingizia mitaji, umbali n.k.
-
Mkurugenzi Wa AMI-TZ Deborah Malaba akiwa akiwa anafanya Usafi (picha na Aziz Mwinuka )

HAPA KAZI TU ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiendelea kufanyiwa kazi,kama inavyoonekana katika picha mkurugenzi wa taasisi isiyokuwa ya kiserekali AMITZ inayohusika na uhamasishaji wa kilimo biashara kupitia vyombo vya habari Deborah Mallaba akiwa sambamba na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Taasisi hiyo imeshiriki kufanya usafi katika maeneo ya Nyakato National wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ambapo wananchi wengi walijitokeza kuunga mkono kauli ya rais kuwa siku ya uhuru itumike kufanya usafi ili kuepukana na magonjwa kama kipindupindu.

Mfanyakazi wa Amitz Jimmy Minja akikusanya taka kwa ajili ya kupelekwa jalalani.(picha na Aziz Mwinuka )
Mkurugenzi msaidizi wa taasisi ya Amitz bw.Agape msumari akiwa na afisa mahusiano bi Linah Mvungi wakiunga mkono kauli ya rais ya kufanya usafi siku ya uhuru.(picha na Aziz Mwinuka )















Afisa ugani wa kata mahina bw Emmanuel akiwa sambamba na wafanyakazi wa Amitz katika kufanya usafi.eneo la dampo (picha na Aziz Mwinuka )





Mkurugenzi wa Amitz Bi.Deborah Mallaba akitoa maelekezo kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. (picha na Aziz Mwinuka
















Wafanyakazi wa Amitz wakisherekea siku ya uhuru kwa kufanya usafi kikamilifu (picha na Aziz Mwinuka )






Wafanyakazi wa Amitz katika picha ya pamoja mara baada ya kumuunga mkono Rais Magufuli                                      (picha na Aziz Mwinuka )


Mkurugenzi wa Amitz akiwa pamoja na wakazi wa wilaya ya Nyamagana mara baada ya kufanya usafi wa kina.           (picha na Jimmy Minja )

-



Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi. 

Utaratibu wa kupandikiza hivi sasa umekuwa silaha ya wakulima kuwakomboa dhidi ya wadudu pamoja na magonjwa, na hili kwa sasa halifanyiki tena maabara kama ilivyokuwa awali na hii inadhibitishwa na yale tuliyojionea Njombe tulipotembelea wakulima.


Kwenye shamba la bwana Bosco Kidenya, ana kitalu chenye zaidi ya miche 1200 ya miparachichi, baadhi ikiwa tayari imeshapandikizwa na mingine ikiwa inasubiri kufikia wakati wa kupandikiza.

  Huyu ni mmoja kati ya wakulima walio wengi wanaofanya kazi kwa karibu na CARITAS Njombe, kuboresha uzalishaji wa parachichi, pamoja na kuboresha kipato cha wakulima ambao wanazalisha matunda na mboga mboga.


Mbinu wanayotumia

Wakulima hukusanya kokwa za parachichi kutoka maeneo ya sokoni; wanachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu hiyo ni safi, haijaathiriwa na magonjwa na itaota. 

Baada ya hapo huchagua zile zenye muundo mzuri na kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya kitalu. Baada ya kuota huziotesha kwenye makopo, au kwenye viriba kisha kuendelea kumwagilia maji mpaka zinapokuwa na umbo usawa wa penseli. Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha unene wa penseli. 

Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.

Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo liwiane na mti linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi kukauka.

Mapandikizi ni lazima yatokane na aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile hass, fuerte  au puebla. Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani mapya.

 wana mkataba na Africado, watahitajikupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya hass.

 Hii ina maanisha kuwa mkulima anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti 5 ya parachichi aina ya hass ili kupata mapandikizi.

Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili magonjwa.

 Wakulima pia wamekuwa na rikodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.

Wakulima ambao wanafanya kazi zao chini ya CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza, wameamua kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye vitalu vyao. 

Hii ni mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima, huku akiwa amewekeza kwa kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu na magonjwa na kuepuka kuwa na mazao yenye ubora wa chini.

Namna ya kupanda

• Nafasi halisi inayohitajika na mmea wa parachichi ili ukae vizuri ni nafasi ya 9m x 9m. Chimba shimo katika vipimo vya 60sm x 60sm kwa 60sm kwenda chini kisha tenga udongo wa juu na wa chini. 

Changanya udongo wa juu na mbolea ndoo moja iliyooza vizuri, pamoja na kiganja kilichojaa cha mbolea ya minjingu.

• Ondoa mche wako kwenye kiriba ulipopandwa. Hii itakuwa rahisi zaidi endapo ulikuwa umenyweshea muda kidogo uliopita. Panda kwa kutumia udongo wa juu uliochanganya na mbolea na uweke mpaka kujaza shimo.

• Mwagilia maji mara baada ya kupanda. Funika mmea mchanga kwa kutumia majani ya migomba au aina nyingine ya majani yanayofanana na hayo, mpaka kufikia kipindi ambacho mmea utatoa majani mapya.


-

Ili kulima matikiti maji inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.

HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi machi mpaka septemba .

UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenye mifuko ya plastiki halafu ndo uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenyewe, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia


UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi

MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi


UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi

MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi.
-