Select Menu

Makala

KILIMO BIASHARA

MKULIMA

‹
›

UFUGAJI

UVUVI

PICHA ZA MAZAO

VIPINDI VYA RADIO

VIPINDI VYA RUNINGA-TV

MUHOGO ni moja ya mazao ya mizizi na lenye umuhimu katika mazao makuu ya chakula baada ya zao la mahindi nchini Tanzania.

Umuhimu wa zao hilo unatokana na uwezo wa kustawi katika mazingira tofauti ya hali ya hewa na rutuba ya udongo. Muhogo unastahimili ukame na hivyo kuitwa zao la kinga ya njaa hasa kunapojitokeza ukosefu wa mvua katika msimu husika.

Zao la Muhogo linatumika kwa kuandaa aina mbalimbali ya vyakula, ikiwa ni pamoja na ugali, chipsi, maandazi, chapati, mkate, keki na biskuti. Pia majani yake hutumika kama mboga maarufu kisamvu.

Aina za muhogo
Kuna makundi mawili ya muhogo ambazo ni muhogo mtamu na mchungu. Katika makundi hayo kuna aina zaidi ya 21 za mihogo zilizothibitishwa na wataalamu wa kilimo nchini. Aina hizo za mihogo hulimwa kwa kuzingatia hali ya hewa na udongo katika kanda husika.

Kwa mujibu wa rekodi za kilimo cha muhogo nchini, kuna kanda nne zinazojihusisha na kilimo hicho. Kuna Kanda ya Pwani inayojumuisha Naliendele, Kiroba, Mkumba, Kibaha na Pwani.

Kanda ya Kati inajumuisha Hombolo, Dodoma, Makutupora na Mumba, Kanda ya Ziwa na Magharibi inajumuisha Mkombozi, Kyaka, Meremeta, Nyakafulo na Fuma ambapo Kanda ya Zanzibar na Pemba inajumuisha Kizimbani, Mahanda na Machui na Kama.

Kutayarisha shamba
Muhogo hustawi zaidi kwenye udongo wa kichanga au ardhi tifutifu yenye rutuba ya wastani. Shamba litifuliwe vyema baada ya kufyeka na kung’oa visiki kabla ya msimu ni vyema matuta yaandaliwe ili kuwezesha ukuaji wa mizizi, kurahisisha uvunaji.

Kutayarisha mbegu
Mbegu zichaguliwe kutoka kwenye miche ya muhogo isiyoshambuliwa na wadudu na magonjwa kama batobato na michirizi ya kahawia. Mbegu hukatwa vipandepande kutoka kwenye muhogo uliostawi vizuri na vitumba vizuri vilivyo karibu na kuondoa sehemu ngumu ya shina na sehemu ya juu kuepuka sehemu laini.

(Sehemu ya katikati ya shina ndiyo inafaa kukata pingili) Pingili/vipande hukatwa kwa urefu wa sentimeta 25 hadi 30 wastani wa vitumba vinane.

Kupanda muhogo
Muhogo hupandwa mwanzoni wa msimu. Pamoja na muhogo kuvumilia ukame, mvua chache hupunguza mazao. Upandaji unaostahili ni kufukia sehemu kubwa ya ya pingili ardhini kwa kuilaza mshazari kidogo (nyuzi 45) ili macho yatakapotoa machipukizi yaelekee juu. Shindilia udongo kando ya pingili.

Nafasi za upandaji nazo zimegawanyika kutokana na aina ya udongo, aina ya muhogo wenyewe na kama muhogo unachanganya na mazao mengine. 

Nafasi za upandaji zilizopendekezwa ni mita moja kwa mita moja ikiwa unapanda mbegu ya muhogo unazaa sana na muhogo wake ni mirefu.

Unapaswa kuacha nafasi ya mita moja kwa sentimeta 90 ikiwa unatumia mbegu ya muhogo unaozaa sana na muhogo wake ni mfupi mnene. Unapaswa kuacha nafasi ya mita 1 kwa sentimeta 75 ikiwa unatumia mbegu ya muhogo unaozaa kwa wastani.

Mbolea
Kwa kuwa muhogo unastawi vizuri katika udongo usio na rutuba Tanzania haina rekodi rasmi kuhusu ushauri wa mbolea inayopaswa kutumiwa katika kilimo cha muhogo.

 Hata hivyo unaweza kutumia kutumia samadi au mboji ili kuuongezea udongo wa shamba uwezo wa kutunza unyevu hasa maeneo yenye udongo wa kichanga.

Palizi
Ni muhimu kufanya palizi katika kilimo cha muhogo na ni vyema palizi ifanyike mara tatu kwa msimu ili kuzuia magugu ambayo husababisha kunyang’anyana lishe muhogo. 
Pia palizi inasaidia kuondoa majani yanayotengeneza maficho kwa visumbufu vya mimea (wadudu na magonjwa).

Kurudisha udongo kwenye mashina wakati wa palizi huongeza mazao.Visumbufu vya muhogo Ingawa muhogo unahimili ukame unaweza kuathiriwa na visumbufu yaani wadudu mbalimbali ikiwa ni Cassava whitefly wadudu weupe wanaoshambulia muhogo, cassava green mites (CGM), wadudu ambao hushambulia majani mapya ya muhogo hasa sehemu za chini na Scales yaani wadudu wanaojishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo.

Visumbufu vingine ni cassava mealbugs yaani wadudu wanaoshambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. 
Athari zake ni kwamba majani yanadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana. Pia visumbufu kama mburumundu, nzige na vidugamba huathiri mihogo.

Visumbufu karibu vyote vilivyotajwa hapo juu vinashambulia muhogo kwa kufyonza majani na kuleta madhara kwa namna tofauti na kusababisha uzalishaji duni wa muhogo Ili kuvidhibiti visumbufu hivyo unapaswa kuwasiliana na mtaalamu wa kilimo aliyepo karibu nawe kwa ushauri wa kina.

Magonjwa
Yapo magonjwa mengi ya muhogo lakini ugonjwa wa Batobato ndiyo unaosumbua sana wakulima hapa Tanzania.

 Ugonjwa wa batobato husababisha majani yakunjamane na kuwa ya njano na mwisho hupuputika na kufanya mmea kudumaa na kushindwa au kutowa mazao hafifu na yasikuwa na ubora, ugonjwa huu huenezwa na inzi mweupe (cassava whitefly).

Kuzuia
Unashauriwa kutumia mbegu za muhogo zinazokinzana na ugonjwa wa batobato (waone wataalamu kwa ushauri).

 Kuvuna Muhogo huanza kukomaa kuanzia mwezi wa nane hadi 12 tangu kupandwa shambani hii kulingana na aina ya mbegu. Uvunaji hufanyika kwa kuchimba na kung’oa shina lote au kutoa baadhi ya muhogo na kuacha shina liendelee pale shambani.
- -

Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini katika ukanda wa bahari ya Mediterania. 

Zao hili hulimwa katika nchi nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C – 24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. 

Joto zaidi ya hapo hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).

Matumizi
Kitunguu hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula, na pia hutumika kama dawa ya kansa ya tumbo, vidonda na majipu.

Ustawi
Zao la vitunguu hustawi katika udongo wa tifu tifu wenye mbolea ya kutosha, ukiwa na uchachu wa udongo (PH) kiasi cha 6 – 6.8.  Udongo wa mfinyanzi haufai kwa zao la vitunguu kwa kuwa hauruhusu viazi vya vitunguu (bulbs) kutanuka.  Hivyo uwezekano wa kupata mazao ni mdogo. Pia udongo wa kichanga haufai kwa zao la kitunguu kwa kuwa hauna mbolea na hivyo vitunguu huwa vidogo sana, jambo ambalo ni vigumu kupata mazao yanayofaa kwa soko.
Zao la kitunguu huhitaji unyevu muda wote wa ukuaji wake. Zao hili lina mizizi mifupi hivyo linahitaji kumwagiliwa maji mara kwa mara.

Aina za vitunguu

Kuna aina mbili za vitunguu ambazo zimezoeleka:
• Vitunguu vya asili kama vile Singida, na Rujewa (aina hii ina rangi ya kahawia iliyopauka).
• Chotara: Hii ni aina ya vitunguu inayojulikana kama vitunguu vya kisasa. Katika kundi hili kuna vitunguu kama Texas grano, Red creole, Bombay red, White granex, na Super rex.

Mgawanyiko

Zao la vitunguu limegawanyika katika makundi mawili. Hii inatokana na uhitaji wa mwanga na ukuaji wake.  Aina ya kwanza inahitaji mwanga kwa saa 8-13 ili kuweza kuchanua na kutoa mbegu.

Aina ya pili inahitaji mwanga kwa saa 13-15 kuweza kuchanua na kutoa mbegu.

Kupanda

Vitunguu hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo husiwa kwenye vitalu.  Kitalu kinaweza kuwa na upana wa mita 1, urefu unategemeana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.

Unaweza kupanda vitunguu kwenye matuta mbonyeo (Sunken bed). Aina hii ya upandaji hutumika kwenye eneo lenye shida ya maji. Upana wa tuta uwe mita moja.

Kupanda kwenye matuta mwinuko (Raised bed) upandaji wa iana hii hutu mika sehemu yenye maji mengi au yanayotuama.

Tahadhari: Maji yakituama kwenye vitunguu hufanya vitunguu kuoza, hivyo kuathiri mavuno.

Nafasi

Vitunguu vipandwe kwa nafasi ya sentimita 7.5 kutoka mche hadi mche, sentimita 12.5 kutoka mstari mmoja hadi mwingine kwenye matuta.

Mbole ya kupandia

Unaweza kutumia mboji, au samadi iliyo oza vizuri kupandia. Baada ya hapo unaweza kuongeza mboji baada ya miezi miwili. Endapo unafanya kilimo kisichozingatia misingi ya kilimo hai, unaweza kupanda kwa kutumia mbolea aina ya NPK (20:10:10) baada ya mwezi na nusu, unaweka mbolea ya Urea.

Palizi

Vitunguu ni zao lenye uwezo mdogo sana wa kushinda na magugu. Hivyo, inabidi shamba liwe safi muda wote wa ukuaji hadi kuvuna.

Uvunaji

Kwa kawaida, vitunguu huchukua muda wa miezi 5-6 tangu kupandwa hadi kuvunwa. Unaweza kuanza kuvuna vitunguu baada ya asilimia 75 ya shingo za vitunguu kuvunjika.  Baada ya kuvuna, unaweza kuweka kwenye madaraja (grades) kwa kufuata ukubwa, rangi na unene wa shingo ya kitunguu. Vitunguu vyenye shingo nyembamba hudumu zaidi, vyenye shingo nene huoza haraka.

Ukataji

Hakikisha kuwa shingo ya kitunguu inabaki kiasi cha sentimita 2. Hii husaidia kuzuia kuoza haraka.

Namna ya kuhifadhi vitunguu

Baada ya kuvuna, hifadhi vitunguu kwenye kichanja chini ya kivuli na uvitandaze vizuri.  Unaweza kuhifadhi vitunguu kwa kufunga kwenye mafungu na kuvitundika.  Vitunguu vikihifadhiwa vizuri vinaweza kukaa hadi miezi minne bila kuharibika, hii hutegemeana na aina ya uhifadhi.

Wadudu wanaoshambulia vitunguu

Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu.  Hawa wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu.

Thiripi
Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe.

Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.

Kimamba
Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.

Minyoo fundo (Nematodes): Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya vitunguu. Hali hii husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa kufyonza maji na chakula kutoka ardhini.

Vidomozi (Leaf minor): Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye ngozi ya jani na kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.

Utitiri mwekundu (Red spider mites): Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu kunyauka.

Funza wakatao miche: Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na hushambulia shina na kulikata kabisa.

Namna ya kukabiliana na wadudu hawa

Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha mzunguko.  Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha mazao jamii ya vitunguu kama vile leaks.

Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni zinatambuliwa kisheria na kibiashara.  Kupanda kwa wakati unaotakiwa; vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya baridi na kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu, au dawa nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo.

Magonjwa yanayoshambulia vitunguu

Purple blotch
1. Purple blotch: Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus). Ugonjwa huu husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya vitunguu.  Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).

2. Stemphylium leaf blight: Hukausha majani kuanzia kwenye ncha hadio kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu na ukungu mwingi.
Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).

Onion yellow draft virus
3. Magonjwa ya virusi (Onion yellow draft virus): Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika, kijani na michirizi myeupe au njano.  Vitunguu hudumaa kwa kiasi kikubwa;Ugonjwa huu husababishwa na kimamba.
Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.

4. Kuoza kwa kiazi (Bulb rot): Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu hutokea vitunguu vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji.  Vitunguu vikishakomaa visimwagiliwe tena.

Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
1. Kuchipua baada ya kuvunwa: Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa kabla ya muda wake.  Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya kuvunwa. Hali hii husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%).  Sehemu ya kukaushia vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa kutosha. Vitunguu vikiwekwa gizani huchipua kwa urahisi.

2. Muozo laini (Soft rot): Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya kukomaa; husababishwa na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya ya uozo.  Kuepuka hilo vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye mwanga na hewa inayozunguka.

Virusi
Unaweza kuzuia vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu.

Vitunguu vinalipa

“Vitunguu vinatofauti kidogo na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuwa si rahisi kukosa soko, na endapo bei si nzuri unaweza kuhifadhi kwa muda ili kusubiri bei iwe nzuri.” Ni maneno ya mkulima Peniel Rodrick (pichani) ambaye amejikita zaidi katika kilimo cha vitunguu kibiashara.  Mkulima huyu kutoka kijiji cha Oloigeruno anasema pamoja na kwamba anazalisha pia mazao mengine, lakini ameamua kujikita zaidi kwenye vitunguu baada ya kugundua siri na namna ya kupata faida zaidi.

Toka aanze kilimo cha vitunguu miaka 12 iliyopita, ameweza kuendesha maisha yake vizuri, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mingine kama ufugaji wa ng’ombe, kujenga nyumba ya kisasa na kuitunza familia yake ya watoto watatu ipasavyo. Pamoja na hayo anasema tatizo kubwa la vitunguu ni magonjwa na wadudu. Anasema si rahisi sana kugundua mara moja kuwa kuna ugonjwa unaoshambulia vitunguu, na mara unapogundua unakuwa umefikia kwenye hali mbaya.
- -

Huu ni ugonjwa unaowashika ng’ombe, kondoo, mbuzi, pamoja na wanyama wa porini kama mbogo, swala na wakati mwingine tembo.

Ng’ombe anapopatwa na ugonjwa wa miguu na midomo huchechemea na asipotibiwa kwa haraka hushindwa kusimama na kula hatimae hudhoofika na hata kufa.

Ugonjwa wa miguu na midomo husambaa haraka kwenye kundi ukiua ndama na kusababisha wanyama kupoteza uzito na uzalishaji wa wengine kupungua.

Namna unavyoambukizwa
Ugonjwa huu unaambukiza kwa kugusana kwa mnyama mmoja na mwingine. Unaweza vile vile kusambazwa na upepo kwenye umbali hata wa kilometa 250. Pamoja na kusambaa kwa umbali huo, ni nadra kwa binadamu kupata ugonjwa huu.

Kwa muongo mmoja uliopita, wastani ugonjwa huu ulikuwa unashambulia kundi mara moja kwa mwaka. Kwa sasa, katika sehemu nyingi za Afrika Mashariki, ugonjwa unatokea mara tatu kwa mwaka. Aidha, jinsi hali ya hewa inavyokuwa ya joto la juu, yanatokea matabaka mapya ya vimelea visababishavyo ugonjwa huu.

• Kuwepo mifugo yenye dalili za mafua, na kuchechemea kwa wakati huo huo.

• Ndama kufa kwa ghafla kutokana na ugonjwa wa moyo.

Tahadhari

Ugonjwa wa miguu na midomo una madhara makubwa kiuchumi hasa ukizingatia kuwa, uzalishaji wa maziwa wa ng’ombe waweza kupungua kwa asilimia 75 kwa maisha yake yote.

Mbali na hayo, ng’ombe badala ya kuzaa kila mwaka au kwa vipindi kama hivyo, anaweza kuzaa kila baada ya miaka miwili au mitatu.

Namna ya kuzuia
Chanjo kwa ajili ya ugonjwa huu husaidia kuzuia isipokuwa gharama yake ni kubwa kwani chanjo hizo zinanunuliwa kutoka nchi za nje na lazima iwe ya kufanyakazi dhidi ya aina nyingi za vimelea. Hata hivyo, jamii inaweza kupanga, na kununua chanjo kwa kushirikiana.

Ugonjwa wa miguu na midomo ni tishio, hasa katika maeneo ambapo mifugo inatumia ardhi ambayo pia inatumiwa na mbogo na nyumbu. 
Ni vyema kwa wale wanaoishi katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa ardhi wanayotumia kulishia mifugo yao si ile inayotumiwa na wanyama pori.

Ugonjwa wa nyumbu (Malignant Catarrhal Fever -MCF)

Nyumbu
Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa zaidi na nyumbu na kuwapata ng’ombe.

Ugonjwa wa Nyumbu ni ugonjwa ambao husababishwa na virusi aina mbili kwa ng’ombe. Aina ya kwanza husambazwa na kondoo na mbuzi wakati aina nyingine husambazwa na nyumbu na pofu.

Aina ya pili ni tatizo kubwa hasa wakati na mahali ambapo nyumbu wanazalia. Virusi vinawaachia watoto wa nyumbu wanapotimiza miezi mitatu baada ya kuzaliwa.

Kwa karne nyingi, ugonjwa wa nyumbu ulikuwa hauwaletei wafugaji madhara makubwa kwa sababu walikuwa wanahamisha mifugo yao kwenda sehemu nyinginezo kila mwaka katika kipindi ambacho nyumbu wanazaliana.

Mpango huu wa kimila wa matumizi ya ardhi umesambaratika, ijapokuwa ni katika miongo michache iliyopita, kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya kutumia ardhi (mashindano) na hivyo ng’ombe na nyumbu kulazimika kupata malisho katika eneo moja hata katika vipindi nyeti ambapo nyumbu wanazaa. Bila kuchukua hatua za tahadhari, ng’ombe na nyumbu wataendelea kula katika eneo moja na hivyo uwezakano

wa ugonjwa wa nyumbu kuongezeka pia ni mkubwa.

MCF eyeDalili
Macho ya ng’ombe yanakosa uwezo wa kupitisha mwanga. Baada ya hapo mnyama anapofuka na kufa.

Kuzuia na kudhibiti
Hadi kufikia sasa, hakuna chanjo wala tiba ya ugonjwa huu isipokuwa suala la udhibiti unawezekana kwa kupitia matumizi mazuri ya ardhi.

Dalili Macho ya ng’ombe yanakosa uwezo wa kupitisha mwanga. Baada ya hapo mnyama anapofuka na kufa.

 Mipango ya matumizi ya ardhi inabidi izingatie mahitaji ya wafugaji na uhamaji wa nyumbu na mazalia yao. Mipango inaweza kuweka eneo tofauti la malisho ya mifugo kwenye majira ya nyumbu kuzaa, ambayo kwa wastani yanaanza mwishoni mwa mwezi Februari hadi Mei.
-

Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda.
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine.

bamiaMatumizi

Bamia hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Aidha majani yake pia  huweza kuchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Lishe

Zao la bamia lina virutubisho vingi ambavyo ni muhimu kwa miili yetu kama;
• Madini ya chokaa ambayo hujenga meno na mifupa
• Husaidia sehemu za viungo mbalimbali vya mwili kama sehemu za magoti, utumbo na macho.

Udongo

Bamia humea na kukua vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha na udongo usiotuamisha maji. Aidha, kama ardhi haina rutuba ya kutosha, ni vyema kuweka mbolea ya mboji au samadi.

Hali ya hewa

Zao hili hustawi katika mita 1,000 kutoka usawa wa bahari na haliwezi kuvumilia hali ya baridi kali.

Uoteshaji

• Shamba la bamia ni vizuri lilimwe mapema kabla ya kuotesha bamia.

Mbegu

• Mbegu bora zenye kutoa mavuno mengi zichaguliwe.
• Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kulowekwa mbegu kwa muda wa siku moja kabla ya kuotesha ili kurahisisha uotaji.
• Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.

Nafasi

Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

Oktra2
Bamia inapotunzwa vizuri humpatia mkulima nafasi nzuri ya kujiongezea pato kwa kuwa hupata bei nzuri sokoni tofauti na bamia ambayo haikutunzwa vizuri.

Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza.

Umwagiliaji

Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini.

Wadudu waharibifu

Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na utitiri mwekundu.

Magonjwa

Magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.

Mambo ya kuzingatia

• Tumia mbegu bora
• Panda kwa nafasi
Bamia fresh• Mwagilia maji ya kutosha
• Palilia shamba vizuri
• Vuna kwa wakati unaotakiwa

Uvunaji

• Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
• Kiasi cha kilo 8,000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
• Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna.

- -

Kambale (Ietalurus Punetaus), ni aiana ya samaki ambao wana majina mengi kulingana na eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu n.k.

kambaleAsili ya samaki hawa ni Amerika ya Kaskazini. Samaki hawa hukua kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa. Aina hii ya samaki hupendwa na watu wengi kwa kuwa nyama yake ina ladha nzuri na ni laini sana.
Samaki hawa huzaliana vizuri zaidi wanapokuwa mtoni au sehemu ambayo wanapata tope. Mfugaji anapokusudia kufuga aina hii ya samaki kibiashara, ni lazima kusakafia bwawa ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababishwa na samaki hawa.

Umbile

Samaki aina ya kambale wana umbo refu, mpana kuanzia shingoni, ingawa kichwa ni kidogo, na upande wa mkia ni mwembamba. Samaki hawa wana rangi ya kijivu na wengine nyeusi.

Kulisha
Unaweza kulisha kambale kwa kutumia unga wa samaki, maharagwe yaliyosagwa, mahindi, mchele pumba, ngano na bidhaa nyingine. Unaweza kujenga mfumo ambao utawawezesha samaki hawa kupata aina mbalimbali za wadudu, pamoja na majani, ili kusaidia wapate mlo kamili.

Ukuaji na uvunaji
Aina hii ya samaki, wakitunzwa vizuri, wanaweza kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri unaoweza kumpatia mfugaji faida nzuri. Unaweza kuanza kuvuna kambale baada ya miezi sita tangu walipopandikizwa kwenye bwawa.

Fikiria soko la samaki kabla ya kuanza kuzalisha

Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha.
Inapofikia wakati wa kuvuna samaki, kiasi kikubwa huuzwa papo hapo bila kufika kwenye soko halisi, jambo linalosababisha kipato kuwa duni. Ni vyema mfugaji akawa na soko maalumu ambalo atazalishia. Unaweza kuzalisha kwa ajili ya shule, hospitali, vyuo, au taasisi yoyote. Halikadhalika jamii inayokuzunguka na taasisi nyinginezo.

Ni vizuri kuzingatia yafuatayo kabla ya kuanza uzalishaji wa samaki

• Fahamu ni aina gani ya samaki inayopendwa zaidi katika eneo ulipo.
• Samaki wanaopendwa wanatakiwa wawe na ukubwa gani.
• Kiasi cha samaki kinachohitajika katika soko ulipo.
• Ni kipindi gani ni kizuri kwa uvunaji wa samaki.
• Ni wakati gani mzuri wa kuuza samaki.
• Je, katika eneo lako kuna mfugaji mwingine anaezalisha samaki kwa ajili ya soko hilo?.
• Bei ya aina ya samaki unaozalisha ikoje?

Wasikilize wateja

Wakati wote mfugaji anapouza samaki, ni lazima kusikiliza kwa umakini, wateja wako wanasemaje.
• Je, wanapendelea samaki unaouza.
• Je, samaki wako ni wadogo sana au ni wakubwa sana.
• Wakija kununua wananunua kwa kiasi gani, kikubwa au kidogo.
• Je, wanapendelea uzalishe zaidi?
• Je, kuna wafanyabiashara wanataka uzalishe zaidi ili nao wanunue.
• Wanataka samaki wawe kwenye ubora gani.
• Wanaridhika na bei unayowauzia.

Fuata haya kwa ufanisi wa soko la samaki

• Hakikisha samaki wako katika hali ya usafi na vyombo salama unapovua tayari kwa kupeleka sokoni.
• Samaki ni bidhaa inayoharibika kwa haraka, hivyo hakikisha unawapeleka sokoni mara tu baada ya kuwavua.
• Hakikisha gharama za usafiri, utunzaji na uhifadhi, zinalipwa kutokana na bei ya soko.
• Kumbuka gharama za uhifadhi wa bidhaa inayoharibika haraka kama samaki ni kubwa, hivyo vua kwa awamu kulingana na mahitaji.
• Unaweza kuongeza thamani ya samaki kwa kufanya mambo ya msingi yanayohitajika kwenye uandaaji wa samaki, kama vile kuparua na kutumbua.
• Unaweza kuwasafisha, na pia kuwakaanga kulingana na soko husika.
Kwa kuzingatia mambo hayo machache, mfugaji anaweza kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza kwenye mradi wa ufugaji wa samaki. Pia ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu ya ufugaji wa samaki, ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Tengeneza chakula cha samaki mwenyewe
 
PAGE 7Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.

Mahitaji

• Pumba ya mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.

Namna ya kuandaa

• Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.
- -

Ufugaji wa samaki kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Mbali na hilo, mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla ya kuanza ufugaji. Moja ya vigezo hivyo ni soko. Si jambo la busara kuanza shughuli yoyote kabla haujafanya uchunguzi na kujua kama kuna mahitaji ya bidhaa unayokusudia kuzalisha. Wafugaji wengi wameanzisha ufugaji wa samaki lakini wakaishia kupata hasara kutokana na ukosefu wa soko. Na wengine wameanguka kutokana na utunzaji mbovu wa mabwawa ya samaki.

Maji
 Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu katika ufugaji wa samaki. Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji. Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki. Wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatika yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Kwa wakazi wa Dar es
Salaam, inawezekana pia kufuga samaki kwenye bwawa, endapo maji yana chumvi ya wastani, na kwa kiwango kinachoshauriwa kitaalamu, basi samaki wanaweza kustahimili, na kukua vizuri.

Bwawa

Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.

Utengenezaji wa bwawa la samaki kwa maeneo yenye udongo wa kichanga kama Dar es Salaam, mfugaji atalazimika kuchimba na kuweka karatasi ya nailoni. Hii, itasaidia kuzuia upotevu wa maji pamoja na kuzuia bwawa kuporomoka.

Ni vyema upande mmoja wa bwawa ukawa na kina kirefu kuliko mwingine. Upande mmoja unaweza kuwa na kina cha mita moja na nusu, na mwingine mita moja. Hii itamsaidia mfugaji kuweza kulihudumia bwawa vizuri, hata kama ni kuingia na kufanya usafi.
Utunzaji wa bwawa

Samaki 1Inashauriwa kufanyia bwawa usafi mara kwa mara, hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Pia ukiacha mimea bwawani itatumia virutubisho kwa kiasi kikubwa na kuondoa hewa ya oxijeni.
Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.

Ulishaji

Wafugaji walio wengi, wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishaji wa samaki. Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha samaki mara mbili hadi mara tatu kwa siku.

Aina ya chakula

Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa. Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi, bali kiwe mabonge madogo madogo, kwa wastani wa tambi.

Magonjwa

Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia, ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu (fangasi), magonjwa yatokanayo na virusi, pamoja na minyoo.

Samaki wanaposhambuliwa na fangasi, huonekana kwa macho kwa kuwa huwa na madoa madoa. Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege.

Pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwa kuwa huzubaa sehemu moja kwa muda mrefu. Magonjwa kwa samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano kwenye bwawa. Hivyo, ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.

Tiba

Tiba iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji, kasha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa, kisha kuwatoa na
kuwarudisha bwawani.

Upatikanaji

Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki Kingolwira Morogoro. Bei ya kifaranga cha Perege ni shilingi 50, na Kambale ni shilingi 150.
- -

Uzalishaji wa maziwa ni biashara nzuri sana na ya kuvutia ambayo huwa na faida nyingi na humfanya mfugaji kuridhika hasa kwa yule anayependa kazi hii. Hata hivyo, ni lazima kuanza kwa kuweka msingi imara hata kabla ya kufikiria ni aina gani ya mbegu utaichukua kwa ajili ya kufuga. Ni vizuri kufahamu kuwa, usimamizi ni moja ya jambo muhimu sana ambalo likifanyiwa uzembe linaweza hata kumbadilisha ng’ombe wa maziwa kuwa na uzalishaji duni kama ngo’mbe wa kienyeji.

Aina mbalimbali za ng’ombe wa maziwa huwa na mahitaji tofauti, hivyo kiwango cha maandalizi yako ni muhimu sana. Unahitajika kufahamu kuwa, unalazimika kufikia mahitaji yako kwa ajili ya lishe, si kwenye mahitaji ya awali tu bali pamoja na mahitaji ya baadaye ya ngo’mbe wako. Suala hili limefanya wafugaji wengi kushindwa kuendelea kutokana na kuwa hujiingiza katika shughuli hii bila kuangalia mambo ya msingi yanayotakiwa pamoja na kuweka mipango thabiti.

Pamoja na kuwa mahitaji yote kwa ajili ya lishe na mambo mengine yako sawa, ng’ombe wa maziwa ni lazima kuzalisha kulingana na umbile lake na uwezo wake kamili. Kama utaweza kumudu kufuga ng’ombe halisi wa maziwa, ni lazima pia utambue kuwa uzalishaji wa juu wa maziwa uhitaji pia usimamizi wa hali ya juu. Kwa maana hiyo, ni vyema kufuga ng’ombe wa kiwango cha kawaida (ikiwezekana chotara) ambaye ataendana na uwezo wako wa kumtunza.

Ni vyema tukaangalia aina mbili za ng’ombe wa maziwa ambao wana uwezo wa kuzalisha maziwa mengi;
 
Ng’ombe aina ya Freshiani (Friesian)
(i) Freshiani (Friesian)

Ng’ombe aina ya freshiani ni rahisi kumtambua kutokana na kuwa na rangi nyeusi na nyeupe, na ni ng’ombe wenye uzalishaji bora wa maziwa. Wanyama hawa ni wakubwa na pia wanaweza kuwa na mabaka meupe na meusi au mekundu na meupe. Ikiwa watalishwa vizuri, freshian aliyefikia umri wa kukomaa huwa na uzito wa hadi kilogramu 550 na urefu wa sentimeta 150 kutoka begani. Mtamba huweza kupandwa, akiwa na umri wa miezi mitano huku akiwa na uzito wa kilogramu 360.

Wakati baadhi ya ng’ombe wakiwa na uwezo wa kuishi kwa muda mrefu, uwezo wa kawaida wa kuishi kwa Freshiani ni miaka sita. Hata hivyo, aina hii ya ng’ombe ni wazalishaji wazuri wa maziwa ambao huweza kuzalisha kilogramu 7800 kwa wastani kwa muda wa siku 360 yakiwa na kiwango cha chini cha mafuta ikilinganishwa na aina nyingine ya ng’ombe.

Aidha, aina hii ya ng’ombe huhitaji ulishaji mkubwa hivyo hushauriwa kwa wafugaji wenye uhakika wa kuwa na lishe bora na ya kutosha kwa mwaka mzima.

Ng’ombe aina ya Ayrshire
(ii) Ayrshire

Aina hii ng’ombe huwa na miraba ya kahawia na nyeupe karibu sawa na aina nyingine ya ng’ombe ambao huelekea kuwa na rangi ya (Mahogany). Ng’ombe hawa huwa na wastani wa kawaida, na uzito wa kilogramu 540 katika umri wa ukomavu. Aidha, humudu aina yeyote ya ufugaji na si rahisi kupata matatizo yeyote ya miguu.

Ayrshire huweza kufanya vizuri katika malisho ya aina yeyote tofauti na aina nyingine ya ng’ombe wa maziwa. Kukiwa na usimamizi mzuri na ulishaji mzuri, wastani wa uzalishaji wa maziwa ni kilogramu 5400 ikiwa na kiwango cha juu cha mafuta ukilinganisha na Freshian. Aryshire ni aina nzuri kwa kufuga hasa kutokana na nguvu aliyonayo pamoja na uzalishaji mkubwa wa maziwa. Ng’ombe wa aina hii, hutambulika kwa kuwa na umbo zuri pamoja na chuchu zake kuonekana kuwa zenye ubora. Aidha, utungaji wa maziwa yake, umefanya maziwa yake kuonekana ni mazuri sana katika uzalishaji wa siagi na jibini.

Maziwa ya Ayrshire yanafahamika kama “maziwa bora ya kunywa” kutokana na uwezo wake wa kuwa na mafuta ya kutosha na kiasi kikubwa cha protini. Kwa mfugaji anayeanza, aina hii ya ng’ombe ni nzuri sana kuanza nayo kasha baadaye kuongeza freshiani baada ya uwezo wako wa kuhudumia kuwa imara. Mifugo ya asili ni ghali sana na ni ngumu pia kuwapata, hivyo basi, njia rahisi kwa wafugaji wa maziwa wanaoanza ni kutafuta ng’ombe bora wa kawaida ambao mara nyingi huwa ni chotara, kisha kuwaboresha kwa kutumia mbinu ya kupandikiza dume bora na mwenye uzalishaji mkubwa. Na hii huhitaji elimu ya kutosha kuhusu uchaguzi wa madume.

*Muhimu: Wakati wa kununua ng’ombe kwa ajili ya kufuga, ni vyema mfugaji ukatambua kuwa, wazalishaji wa maziwa mara nyingi hawauzi ng’ombe wao wenye uzalishaji mzuri, badala yake huuza wale ambao hawazalishi kwa kiwango kizuri, wale wenye matatizo kama kutokushika mimba, wenye matatizo ya joto na wale ambao hushambuliwa na magonjwa mara kwa mara. Kwa maana hiyo, pamoja na aina ya ng’ombe unayehitaji kununua, ni muhimu sana kuwa mwangalifu usije ukanunua ng’ombe mwenye shida yoyote kwani hapo ndipo mwanzo wa uzalishaji wako kuja kuwa wa matatizo na kutokufikia lengo.

Banda na nafasi kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa

banda smart.PG - CopyKabla mfugaji hajafikiria kuhusu makazi ya ng’ombe wake, ni vyema sana kujiuliza ni kiasi gani cha mifugo utahitaji kuwa nao baada ya miaka kadhaa hivyo kukuwezesha kutenga nafasi ya kutosha kwa ajili ya mifugo utakayoleta.

Njia rahisi ya kulitambua hilo, ni kujiuliza ni kiasi gani cha mifugo ungependa kuwa nao baadaye na ni kiwango gani cha uzalishaji wa maziwa ungetarajia kufikisha kutoka kwa ng’ombe wako.

Swali la kwanza, ni muhimu sana kwa mfugaji kujiuliza, kwani kiwango cha mifugo hutokana na uwezo wa kiwango cha lishe utakachohitajika kulisha mara kwa mara. Kwa kawaida, ekari moja ya ardhi hutoshea kulisha ng’ombe wa maziwa aina ya Freshiani mmoja au Jesrey wawili tu.

Ng’ombe wa maziwa mmoja (Fresian, Guernsey, Jersey) kiasi cha tani 5 ya lishe ya majani mabichi au majani makavu kwa mwaka. Hii ni sawa na kilogramu 25,000 za matete au kiasi cha majani uliyoyaotesha kwenye ekari moja. Pamoja na usimamizi mzuri wa malisho ya nyasi, au mchanganyiko wa malisho kama mikunde au mimea kama desmodium, ni dhahiri kuwa bado utahitajika kuwa na angalau ekari ya ziada 0.75 ya eneo ili kuweza kulisha ng’ombe wako vizuri.

Kwa ujumla, ng’ombe wa maziwa huhitaji lishe kiwango kikubwa kuliko ng’ombe wa nyama, na mara nyingi huwa na uzalishaji mkubwa pale ambapo ubora wa lishe ni wa hali ya juu. Hali kadhalika, kama utazalisha malisho yako mwenyewe, bado utahitaji njia nyingine ya ziada ya kupata lishe ikiwa itatokea tatizo lolote katika malisho.

Jedwahi hili huonesha kiwango cha lishe kinachohitajika kwa aina mbalimbali ya ng’ombe wa maziwa, pamoja na ardhi kwa ajili ya kuzalishia malisho.
Jedwali

Ufugaji wa ndani

Katika ufugaji wa ndani, ng’ombe wanahitajika kuwekwa kwenye hali ya usafi, na makazi yao yawe na ulinzi wa kutosha na yenye kuwapatia uhuru. Wafugaji walio wengi wamekuwa wakiwekeza fedha nyingi katika kuwajengea mifugo, na mwishoni kuishia
kukosa fedha kwa ajili ya kulishia mifugo hiyo. Mfugaji anayeanza, anashauriwa kujengea mifugo yake makazi mazuri na ya gharama nafuu na baadaye kuendeleza mabanda hayo kutokana na mapato yanayopatikana.

Mambo ya kuzingatia katika ujenzi wa mabanda

Nafasi: Ng’ombe mkubwa anahitaji kuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili ya chakula, kupumzika pamoja kufanya mazoezi jambo ambalo wafugaji walio wengi hawazingatii na badala yake huweka mifugo yao katika nafasi ndogo ambayo mwishoni hudidimiza ukuaji wa mnyama na uzalishaji kwa ujumla. Kwa mantiki hiyo, ng’ombe mmoja mkubwa anahitaji mita za mraba 8 mbali na eneo lake la kupumzikia. Njia rahisi ni kutenga eneo hili mbele ya zizi/banda. Kumbuka, unapokuwa na nafasi kubwa, ndipo unapotengeneza uzalishaji mzuri.

Paa: Ni vyema kukawa na paa kwa ajili ya kuilinda mifugo dhidi ya upepo, mvua pamoja na jua kali. Hakikisha paa linakuwa juu, ili kuipa uhuru mifugo yako kutembea ndani ya banda bila tatizo lolote. Hakikisha mteremko wa paa hauwezi kuathiri sehemu ya mifugo kupumzika na sehemu ya lishe hasa kwa kuruhusu maji kuingia katika sehemu hizo.

cow beddings 
Ni muhimu ng’ombe kuwa na mahali safi pa kulala
Sakafu: Hakikisha sakafu inakuwa na mfumo mzuri wa mifereji kwa ajili ya kuruhusu maji na mkojo kupita hivyo kuwaweka mifugo katika hali nzuri. Unaweza kutengeneza sakafu ya simenti ambayo ni rahisi kusafisha. Hata hivyo kwa kuwa inagharimu fedha, mfugaji anaeanza, anaweza kutumia udongo wa mfinyanzi au aina nyingine ya udongo mgumu kutengeneza sakafu. Endapo utasakafu banda, sakafu isiwe inayoteleza kwa kuwa ng’ombe wanaweza kuteleza na kuumia. Sakafu iwe na mwinuko kidogo na mwinuko uelekee sehemu ya kutiririshia mkojo na kutolea kinyesi.

Matandiko: Eneo ambalo mifugo hupumzikia, ni vyema kukawa na matandiko. Unaweza kutumia malighafi ya aina yeyote kavu ambayo huweza kunyonya mkojo na samadi. Matandiko hayo ni lazima kubadilishwa mara kwa mara.

Vihondi vya maji na chakula: Hakikisha kuna vihondi vya kutosha kwa ajili ya chakula na maji. Mabanda ni vyema yakawa karibu na vyanzo vya upatikanaji wa maji safi na salama. Kwa wastani, ng’ombe mmoja anahitaji kunywa maji kiasi cha lita kati ya 50 au 80 kwa siku sawa na ndoo 5 hadi 8 za maji (za ujazo wa lita 10).

Shimo la mbolea: Mifugo inayolishwa vizuri hutoa samadi nyingi hivyo huweza kuwa tatizo kwa watu wanaokuzunguka hasa ikiwa inatapakaa kila mahali na kusababisha kuwepo kwa harufu mbaya. Kama utafuga mifugo mingi katika eneo dogo bila kuwa na sehemu maalumu ya kuweka mbolea inayotokana na mifugo hiyo, basi ni dhahiri kuwa utasababisha kutokuelewana na majirani, lakini pia kutasababishia wanyama kukaa katika hali ya usumbufu. Ni vyema kuandaa shimo maalumu kwa ajili ya samadi hasa kwa ufugaji wa ndani, kabla ya kutumia kwa ajili ya kuweka kwenye mashamba ya malisho.

Namna ya kuanza ufugaji kwa urahisi

Kabla ya kuamua kufanya biashara ya uzalishaji wa maziwa, maandalizi mazuri ni moja ya sababu itakayokupa mwanga kufanikiwa au kutokufanikiwa. Hata kabla ya kuwaza nia aina gani ya ng’ombe utanunua, ni lazima kufikiri kwanza ng’ombe huyo utamlisha nini.

Fikiria lishe, fikiria nyasi

Ili kufuga ng’ombe, ni lazima uwe na lishe ya kutosha. Huwezi kumuendeleza ng’ombe kuzalisha wakati hauna lishe bora ya kutosha, ikiwa ni pamoja na nyasi, mikunde na majani ya nafaka. Moja ya njia nzuri ya kuzingatia ni nyasi. Mfugaji anayeanza, ni lazima kuzingatia haya kwa ajili ya lishe;

• Hakikisha unatunza nyasi za asili zilizopo katika shamba lako la malisho
• Ongeza kwa kuotesha majani mengine mapya katika shamba lako
• Nunua malisho ambapo unaweza kuswaga mifugo yako kwenda kula
• Kodisha au nunua eneo kwa ajili ya kuotesha malisho kisha kukata na kupeleka kulishia mifugo

• Nunua majani kutoka kwa watu wanye malisho au wanaofanya bishara ya kuuza majani yaliyokatwa tayari.
-
Dairy cow - Copy

banda smart.PG - Copy

Ndizi ni zao ambalo limepokelewa na wananchi wa wilaya mbalimbali hapa nchini na kwa baadhi ya jamii hakuna chakula kingine isipokuwa ndizi ambacho ndicho chakula chao kikuu.

migomba 2Katika miaka iliyopita, mikoa inayolima migomba kama vile Kagera na Kilimanjaro, zao hili lilikuwa likistawi vizuri sana na mikungu ya ndizi ilikuwa mikubwa na mizuri kutokana na udongo kuwa na rutuba ya kutosha. 

Ardhi katika kipindi hicho ilikuwa tele na rahisi kupata maeneo mapya yenye mboji hasa yale yaliyokuwa yakipatikana baada ya wakulima kukata miti na kuotesha migomba. Baada ya kipindi hicho, kilimo cha migomba kilianza kuwa na matatizo makubwa kama yafuatayo;

Rutuba ya udongo kupungua

Hii inatokana na kustawisha migomba katika shamba lilelile mwaka hadi mwaka bila kuongeza mbolea ya aina yoyote, hasa mboji na samadi. Mvua zinazonyesha huondoa udongoni vyakula vya migomba. Upandaji wa aina mbalimbali za mimea katika shamba moja huondoa aina mbalimbali za vyakula vya migomba.

Mabadiliko ya hali ya hewa

Migomba huhitaji sana maji. Kwa bahati mbaya siku hizi mvua hazinyeshi kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma. Hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na uteketezaji wa misitu ya asili na misitu ya kupanda. Matokeo yake ni migomba kukosa maji ya kutosha. Mbali na tatizo hili, upepo mkali na mvua za mawe huharibu mashamba mengi ya migomba.

Upungufu wa wafanyakazi

Huko nyuma, katika baadhi ya mikoa, palikuwa na wakulima ambao walianzisha mashamba ya migomba na kuyatunza kwa msaada wa vibarua. Kwa bahati mbaya katika miaka ya hivi karibuni vibarua wa aina hii hawapatikani. Matokeo yake ni kuwa wenye mashamba makubwa kiasi wamepungukiwa nguvu kazi. Hii imesababisha sehemu kubwa ya mashamba yao kutokutunzwa vizuri.

Watu wenye uwezo kutokufanya kazi za shamba

Kuna vijana wengi wanaomaliza elimu ya msingi kila mwaka, huku taifa na wazazi wao wanategemea warudipo majumbani wasaidie wazazi wao kwa kushiriki kutunza mashamba yao. Lakini hii sivyo ilivyo kwa siku hizi, nguvu yao ya kazi za shamba imepungua sana na wengi wa wazee hao wamezeeka sana na afya zao sio nzuri. Matokeo yake ni kuwa familia nyingi zimezungukwa na mashamba ya migomba na kahawa yasiyotoa tena mavuno mazuri.

Wanyama waharibifu

Katika baadhi ya vijiji lipo tatizo la wanyama waharibifu mfano nguruwe (ambao huharibu mashina ya migomba) nyani na tumbili ambao hula matunda ya migomba. Tatizo hili ni kubwa katika sehemu mbalimbali za nchi yetu zinazostawisha migomba kwa wingi.

Kutojua kanuni za kilimo cha kisasa

Wakulima walio wengi, hawajui kanuni za kilimo cha zao la migomba, yaani kulima kwa kitaalamu. Kwa mfano wakulima wengi hawajui namna ya kudhibiti vifukusi vya migomba na magonjwa mengine.

Upungufu wa ardhi inayofaa 
Siyo kila sehemu ya ardhi inaweza kustawisha aina muhimu za migomba kwa wingi na kwa urahisi. Sehemu nyingi zinazofaa sana kwa kustawisha migomba ni zile ambazo kwa sasa zinastawisha zao hilo. Kwa bahati mbaya au nzuri, sehemu hizo zina watu wengi mno kwa kila eneo la kilometa ya ardhi na tayari kuna upungufu wa ardhi kwa ajili ya upanuzi wa kilimo. Hii ina maana kwamba uzalishaji wa ndizi nyingi zaidi hauwezi kufikiwa kwa kuongeza maeneo ya migomba (maana ardhi haipo) bali kwa kuongeza ufanisi wa uzalishaji.

Kutokuwepo kwa mifumo mizuri ya uuzaji wa ndizi
Hakuna utaratibu maalumu wa kuuza ndizi kama ilivyo kwa mazao mengine kama vile kahawa, tumbaku, pareto, nafaka na kadhalika yanayoshulikiwa na vyama vya ushirika na bodi za mazao.

Usafirishaji mbaya
Tatizo lingine linalokabili kilimo cha migomba ni usafiri mbaya katika baadhi ya vijiji na wilaya hasa vilivyo mbali na miji ambayo ndiyo yenye wanunuzi wengi.

Kupuuzwa kwa utafiti
Utafiti kuhusu mbinu mbalimbali za kustawisha migomba pia ulidharauliwa kwa muda mrefu ukilinganisha na mazao makuu mengine, hasa yale yanayojulikana kama mazao ya biashara. Hii imesababisha zao hili libaki nyuma kiutafiti na matokeo yake ni kuendelea kukumbwa na matatizo ambayo yangetatuliwa mapema.

Uzalishaji bila uchaguzi sahihi wa dume ni kufanya kazi kwa kubahatisha
Tunaangalia uchaguzi wa dume mzuri kwa uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa, pamoja na aina ya malisho ambayo mfugaji anaweza kuyatumia kuweza kukabiliana na changamoto ya malisho kwa ng’ombe.

Wafugaji wengi wamekuwa wakipata ng’ombe wanaozalisha kidogo na kwa kiwango cha chini kutokana na kuangalia ukubwa wa gharama ya mbegu wakidhania kuwa ndiyo upatikanaji wa ng’ombe bora. Vinasaba husaidia kwa kiwango kikubwa katika kupata ng’ombe mzuri wa maziwa.

Kuwepo kwa ongezeko la uzalishaji wa maziwa hutegemeana na vitu viwili ambavyo ni kuboresha mifugo kwa kufanya uchaguzi sahihi wa kizazi pamoja na usimamizi mzuri unaojumuisha lishe kamili, malazi mazuri, upatikanaji wa maji, kuwa karibu na wanyama pamoja na utoaji wa kinga na tiba dhidi ya magonjwa.

Vinasaba pamoja na usimamizi mzuri ni vitu viwili vinavyotegemeana. Bila kuwa na uzao mzuri, uzalishaji wa wanyama pamoja na usimamizi utakuwa wa hali ya chini sana, na bila usimamizi mzuri wanyama bora hawawezi kuonesha ubora wao katika uzalishaji.

Uzao mzuri humpa nafasi kubwa mfugaji kutambua sifa na uzalishaji utakaopatikana katika uzao ujao. Endapo mfugaji atafanya uchaguzi mbaya basi ni hakika atakuwa na uzalishaji hafifu wa maziwa, kuzorota kwa afya ya mnyama pamoja na maisha mafupi.

Muda wa kufanya tafiti

Wafugaji wengi wamekuwa wakifikiria mbegu pale tu ng’ombe anapokuwa tayari anahitaji kupandwa na matokeo yake ni kuwa, kutokana na haraka ya kutaka kumhudumia ng’ombe huyo, basi mfugaji atakuwa tayari kuchukua mbegu yoyote ile atakoyopatiwa na wataalamu. Kwa mantiki hiyo, hakuna muda mfugaji atatumia kuchunguza aina ya dume aliyetumika kupatikana kwa mbegu hiyo na badala yake, gharama hutumika kwa kiasi kikubwa kuonesha uwezo wa dume huyo.

Wafugaji wengi hufikiri kuwa kitendo cha mbegu kuuzwa kwa gharama kubwa ni moja ya njia ya kutambua ubora wa dume. Wauzaji wengi wamekuwa wakitumia njia hii kuwadanganya na kuwarubuni wafugaji.

Ni muhimu sana kwa mfugaji anaelenga kuzalisha maziwa kusoma na kuelewa taarifa zote muhimu zilizotolewa kuhusu aina ya dume husika. Ili kufanikiwa katika uzalishaji wa maziwa, ni muhimu kwa mfugaji kuwa makini na kulichukulia kwa uzito suala la uchaguzi wa dume na kuelewa nini kinahitajika bila kubahatisha. Mfugaji ni lazima atambue kuwa, dume huchangia asilimia 50 ya kinasaba katika uzao wake hivyo ni muhimu sana kujua sifa za dume unayemchukua kwa ajili ya uzalishaji. Pia ubora wa maziwa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya dume aliyetumika. Dume wa maziwa hutambulika kwa kuangalia kiwango cha maziwa yanayozalishwa na ng’ombe aliyepandwa na dume huyo na mtamba aliyezaliwa na ng’ombe huyo ambapo dume huyo husambaza sifa ya maziwa kutoka kwa ng’ombe huyo hadi kwa mtamba.

Elewa maelekezo yaliyopo kwenye kabrasha la mbegu

Kielelezo cha vinasaba hutumika kupima uwezo wa mnyama kusambaza vinasaba vyake kwenda kwa uzao ujao. Katalogi huwa na taarifa muhimu ambazo zitamsaidia mfugaji kufanya uchaguzi mzuri wa dume ili kuwa na uhakika wa kuendeleza kizazi baada ya kingine.

- -

Cabbage is grown virtually everywhere in the world. Its nutritional values and health-giving qualities make it a very popular vegetable with a great future. Within the main types – white, red and savoy – there is great diversity. The Rijk Zwaan range also comprises many kinds and sizes.

Our cabbage types

Red cabbage
Savoy cabbage
White cabbage
Growing popularity
Rijk Zwaan has a leading position in early white cabbage and red cabbage. Our storage varieties are gaining fast in popularity. We have varieties for the fresh market, varieties with specific traits for the processing industry and varieties that are suitable for both. With different sizes of headed cabbage, several sales channels and markets can be served.

Resistance breeding
Our varieties are characterised by a good field life, reliability and optimal performance in and out of storage. Diseases and pests are a major attention point for growers, so Rijk Zwaan gives a lot of attention to resistance breeding. Specific research facilities around the world enable us to test our breeding material in the most extreme conditions.

Changing wishes
Rijk Zwaan is always up-to-date with consumer trends. Cabbage does not just taste good, it is also healthy because of its specific phytochemicals. Thanks to its excellent storability, cabbage is also popular with the processing industry. This industry‘s specific demands determine to an ever greater degree what direction cabbage will take and are an important guideline in Rijk Zwaan’s breeding work.
                                                        Viazi mviringo (Viazi Ulaya )
Kupanda kwa bei za bidhaa sokoni kumefanya baadhi ya watumiaji wa bidhaa hizo kulalamikia mamlaka husika kutozingatia mfumuko huo wa bei kwa watumiaji wake.
-
MBINU SITA ZA KUKIFANYA KILIMO KIWE NA TIJA KIWAVUTIE
WATANZANIA WENGI