GREEN HOUSE (KITALU BANDA )
Ni kijumba au nyumba maalum ambayo hujengwa kwa ajili ya kilimo cha matunda ,mboga mboga ili kuepusha muingiliano wan je na ndani ,kwa mfano wadudu au bacteria mbalimbali ambao wanafanya mmea kuoza ukiwa shambani ,pia mionzi ya jua haliwezi kuingia moja kwa moja katika mmea .na mimea inayopandwa ni ile ambayo hutambaa na pia huweza ukavuna wakati wote mpaka utakapoamua kuing’oa na kupanda mingine mifano ya mimea ambayo unaweza kuotesha ni pamoja na pilipilihoho ,matango ,nyanya na mingine inayotambaa.
Watu wengi wanajiuliza green house au kitalu banda inatumikaje .kwa mujibu wa mkulima ambaye anatumia green house bwana Godfrey Majura amesema kwamba ni kitendo cha kutumia eneo dogo katika kuotesha mmea lakini mwisho wa siku ukapata mazao mengi kutokana na mimea hiyo.unaweza kuotesha eneo dogo lenye 8m kwa 18.
![]() |
Kitalu Banda |
Eneo lenye 8m unaweza kupanda miche zaidi ya 480 katika kuvuna unapata zaidi ya tani 12 na mche mmoja wa mmea aidha kama ni wa nayanya unaweza ukatoa kg 25.
Kilimo hichi cha green house hakihitaji maji mengine tofauti na kumwagilia kutokana na kuwa mvua inakuwa na baadhi ya gesi zitokazo katika viwanda kwahiyo katika kitendo cha evaporation ili mvua inyeshe lazima hizo gesi ziwepo kwa hiyo ikingia katika ile mimea inaweza kuoza na kuharibika ,na endapo mvua ikinyesha wanatumia vifaa maalum kuzibia katika yale matundu ili maji ya mvua yasipenye katika mimea hiyo.
Ina mabomba yake maalum ambayo husimikwa kwa chini ,lakini kuna mirija ambayo huchomekwa kupitia yale mabomba ,mirija hiyo husambazwa kwa mstari mnyoofu kufuatana na mmea jinsi ulivyopandwa ,pia mirija hiyo ina plastic maalum kwa ndani ambavyo inacontroll maji kwa kiasi unachotumia .
Kabla ya kuamua kuweka green house ni lazima kujua historia ya hilo eneo kuwa siku za nyuma kulikuwa kunalimwa ninui .ili kuepuka kulima mazao mengine na yasiote kutokana na historia ya eneo hilo .
Na pia unashauriwa kutumia mbolea kulingana na aina ya udongo na mbole aambayo inatumika katika green house inaitwa anna hii inatumika kwa kilimo cha mmea wowote katika green house (kitalu banda) .
Pia bwana majura alisema kuwa katika green house kwa nje ya kitalu hicho lazima uchimbe kishimo hicho utaweka umekisakafia cement ambapo ndani ya kishimo utaweka maji ambayo utakuwa umeyachanganya na dawa ,ambapo mkulima au mtu yeyote akiwa anaingia ndani ya kitalu hicho lazima anawe mikono yake pale pamoja na miguu ili kuepusha bacteria ambao watakuwa katika mikono pindi utakapokuwa umeshika mimea ile na miguu pindi utakapokuwa umekanyaga eneo hilo (kitalu ).
Unatakiwa pindi unaotesha mazao yako uwe umeandaa kamba maalum ambazo utakuja kufungia mimea hiyo kwa juu pindi yakianza kupanda ju ili kusaidia mimea iendelee kutambua juu zaidi na kuzaliana kwa wingi .
Faida ya kutumia green house inasaidia uzalishaji inasaidia uzalishaji wa muda mrefu ambapo hata kama utakuwa umevuna kwa mara ya kwanza utaendelea kuvuna mpaka utakapoamua kung’oa mimea ile na kuotesha upya.
Pia inawahi kukomaa mapema kulinganisha na kilimo cha kawaida ,na pia ni faida zaidi kutokana na kuwa mche mmoja unazaa takribani kg25.
Kwa hasara zake ni kuwa ukishindwa kutimiza masharti ya umwagiliaji unaweza ukafanya mimea ikafa kabla ya wakati kwani humwagiliwa kwa masaa mawili asubuhi na jioni.pia kushindwa kuonana na mtaalam wa kilimo pindi mazao yanapoleta matatizo au kupata magonjwa .
Unashauriwa kupunguzia majani katika mmea ili kufanya ule mmea kuendelea kupanda juu zaidi na kuzaa mazao mengi zaidi.
No comments