Select Menu

Makala

KILIMO BIASHARA

MKULIMA

UFUGAJI

UVUVI

PICHA ZA MAZAO

VIPINDI VYA RADIO

VIPINDI VYA RUNINGA-TV

» » UFUGAJI WA KUKU NI UTAJIRI WAHARAKA,MAGONJWA NI KIKWAZO KIKUBWA.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post


Ufugaji kuku wakienyeji una faida kubwa zifuatazo; kuanzisha mradi hakuhitaji mtaji mkubwa sana, Kuku wa kienyeji hawahitaji eneo kubwa sana, kuku wa kienyeji wanastahimili mazingira magumu, Kuku wa kienyeji hawaugui mara kwa mara.

aidha kuku wa kienyeji wana soko kubwa sana, kuku wa kienyeji ana bei kubwa sokoni,Mayai ya kuku wa kienyeji ni mazuri sana, Mayai ya kuku wa kienyeji yana soko kubwa.
Faida ya kuku wa mayayi huanza kuonekana pale mfugaji anapokuwa na kuku 500 ambapo anakuwa na uhakika wa kukusanya trei 10 za mayai kwa siku.

Ukiweza kukusanya kiasi hicho cha mayai ya kienyeji unakuwa na uhakika wa kuuza kati ya shilingi 900 hadi 12000 kwa trei moja sawa na shilingi 90,000 kwa siku.

Hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja kama mfugaji atakuwa anauza kwa shilingi 90,000 ana  uhakika wa kuvuna kati ya shilingi milioni 2,700,000 hadi  milioni 3,60,000 kwa mwezi.
Pesa ambayo hata kama akitoa nusu yake kwa ajili ya kulipia gharama ya chakula na dawa bado mfagaji ana uhakika wa kubaki na kipato kikubwa zaidi ya wafanyakazi walioajiliwa au wafanyabiashara zingine   

CHANJO
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali

MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji

CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia

MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
 Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga.

Pia hutupatia protini,Kinyesi cha kuku ni mbolea safi pia ni kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga.

Gharama za kuanzisha na kuendeleza miradi ni nyepesi, kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika.

Jogoo hutumika kama saa inapowika,manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro.

Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa.

Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu.

 Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu.

 Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje  huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%).

TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya.

 Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.

 Kinyesi chaweza kuwa na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa muda.

 Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.

Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1 kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga).

 Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Wadudu
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi.

 Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku  150).

 Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.

Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa wingi.

 Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa. Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu.

 Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo.

 Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili

About Agri-business media initiative in Tanzania

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply