Mkurugenzi Wa AMI-TZ Deborah Malaba akiwa akiwa anafanya Usafi (picha na Aziz Mwinuka ) |
HAPA KAZI TU ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiendelea kufanyiwa kazi,kama inavyoonekana katika picha mkurugenzi wa taasisi isiyokuwa ya kiserekali AMITZ inayohusika na uhamasishaji wa kilimo biashara kupitia vyombo vya habari Deborah Mallaba akiwa sambamba na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Taasisi hiyo imeshiriki kufanya usafi katika maeneo ya Nyakato National wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ambapo wananchi wengi walijitokeza kuunga mkono kauli ya rais kuwa siku ya uhuru itumike kufanya usafi ili kuepukana na magonjwa kama kipindupindu.
![]() |
Mfanyakazi wa Amitz Jimmy Minja akikusanya taka kwa ajili ya kupelekwa jalalani.(picha na Aziz Mwinuka ) |
![]() |
Mkurugenzi msaidizi wa taasisi ya Amitz bw.Agape msumari akiwa na afisa mahusiano bi Linah Mvungi wakiunga mkono kauli ya rais ya kufanya usafi siku ya uhuru.(picha na Aziz Mwinuka ) |
Afisa ugani wa kata mahina bw Emmanuel akiwa sambamba na wafanyakazi wa Amitz katika kufanya usafi.eneo la dampo (picha na Aziz Mwinuka ) |
Mkurugenzi wa Amitz Bi.Deborah Mallaba akitoa maelekezo kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. (picha na Aziz Mwinuka |
Wafanyakazi wa Amitz wakisherekea siku ya uhuru kwa kufanya usafi kikamilifu (picha na Aziz Mwinuka ) |
Wafanyakazi wa Amitz katika picha ya pamoja mara baada ya kumuunga mkono Rais Magufuli (picha na Aziz Mwinuka ) |
Mkurugenzi wa Amitz akiwa pamoja na wakazi wa wilaya ya Nyamagana mara baada ya kufanya usafi wa kina. (picha na Jimmy Minja ) |
No comments