Select Menu

Makala

KILIMO BIASHARA

MKULIMA

UFUGAJI

UVUVI

PICHA ZA MAZAO

VIPINDI VYA RADIO

VIPINDI VYA RUNINGA-TV

» » » MFUMUKO WA BIDHAA SOKONI NI KIKWAZO KWA WATUMIAJI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

                                                        Viazi mviringo (Viazi Ulaya )
Kupanda kwa bei za bidhaa sokoni kumefanya baadhi ya watumiaji wa bidhaa hizo kulalamikia mamlaka husika kutozingatia mfumuko huo wa bei kwa watumiaji wake.

Hayo yamesemwa na baadhi ya watumiaji wa bidhaa ya viazi mviringo na mchele wakati walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari wa Ami-TZ katika soko la Igoma mkoani Mwanza.
Wamesema kuwa mwanzoni kwa bidhaa kama viazi walikuwa wakinunua kwa kg1 sh 500 lakini ilifika na kuwa sh 700 kwa kg1 hali ambayo inawapa changamoto katika ununuaji.
Aidha Julieth Chimamy ambaye anafanya biashara ya chakula amesema kuwa kufumuka kwa bei ya vitu hivyo sokoni kumefanya biashara ya chakula kuwa ngumu kutokana na kuwa mwanzoni mchele ulikuwa 1500 kwa kg1 ila umekuja mpaka 1800 kwa kg1 hali ambayo inafanya soko la chakula linakuwa gumu.



'' Kiukweli kupanda kwa bei ya mchele kunafanya sisi wafanyabiashara tuwe katika mazingira magumu kwasababu unatakiwa katika kg5 utoe sahani 35 na wateja wamezoea sahani sh1000,sasa ukiwapandishia bei na wao hawanunui hali ambayo ni hasara''.alisema bi Julieth Chimamy mmojawapo wa wafanyabiashara katika eneo la Nyakato mjini Mwanza.
Pamoja na hayo pia wana AMI-TZ waliweza kuzungumza na mtumiaji mwingine wa bidhaa hizo bw Emmanuel Christopher ambaye ni mtumiaji wa viazi katika ukaangaji wa chipsi ambaye alisema kuwa ,mwanzoni viazi vilikuwa ni sh500 kwa kg1 ila baada ya kupanda ilikuwa pia ni hasara kwa sababu ya wateja kuzoea chipsi 1500 badala ya 2000,hali ambayo inakufanya uuze kwa hasara ili kumridhisha mteja.
Hata hivyo wauzaji wa sokoni wamesema kuwa kupanda kwa beiza bidhaa sio kosa lao ila ni kutokana na ushuru kuongezeka na pia mizigo yao kuchukulia mbali.
Sambamba na hayo mwenyekiti wa soko hilo Bwana Mawazo Mazige amewaomba wananchi au watumiaji wa bidhaa kuwa wapole kutokana na kuwa hiki ni kipindi cha kiangazi kwa hiyo mazao yanakuwa ni machache na bidhaa kupanda bei ila mvua zikiwepo mazao yataongezeka na kukidhi mahitaji maalum kwa bei sahihi.

About Agri-business media initiative in Tanzania

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply